MAJALIWA AFUTURISHA WAUMINI MBALIMBALI WA DINI YA KIISLAM KATIKA IFTAR MAALUM DAR ES SALAAM

 MAJALIWA AFUTURISHA  WAUMINI MBALIMBALI WA DINI YA KIISLAM KATIKA IFTAR MAALUM DAR ES SALAAM

 

Dar es Salaam 

Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa,Leo amewafuturisha mamia ya waumini wa dini ya kiislam pamoja na viongozi katika tukio maalum la Iftar lililofanyika leo Machi 10, 2025 jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena. 

Tukio hilo limeandaliwa na Mshauri wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Tukio hilo la Iftar limewakutanisha viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini, wadau kutoka sekta binafsi pamoja na wageni wengine mashuhuri waliokusanyika kwa ajili ya kushiriki futari na kuimarisha mshikamano na upendo katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Hata hivyo katika tukio hilo walihudhuria makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo watoto wanaoishi katika mazingira magumu 

Waumini wa dini ya kiislamu duniani kote wapo katika kipindi Cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Comments