SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAJA NA SWIFTPACK,LAINGIA MKATABA NA MADEREVA DAR
Shirika la Posta Tanzania leo limeingia mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati yake na chama cha madereva wa bajaji na pikipiki wilaya ya Kinondoni kupitia biashara ya swiftpack ambayo itakuwa inatoa huduma ya usafirishaji mtandaoni.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utilianaji saini wa makubaliano hayo,Mkurugenzi wa Masoko na mauzo wa shirika hilo Ferdinand Kabyemela amesema kuwa mashirikiano hayo yamekuja kama suluhisho la sekta ya usafirishaji wa bodaboda na bajaji, ambapo kupitia swiftpack sasa wateja wataagiza usafiri huo kwa urahisi zaidi na unafuu wa gharama kwa kuwa na makato ya chini kabisa.
Amesema kuwa Kwa sasa watatumia swiftpack bila gharama zozote za internet kwa hiyo mteja na dereva watatumia huduma hiyo bila kuwa na internet ambapo pia madereva hawatakatwa gharama kubwa za uendeshaji kama wanavyofanyiwa na makampuni mengine binafsi.
Amesema kupitia mfumo wa swiftpack madereva zaidi ya Milioni 5 wanaweza kusajiliwa kwa wakati mmoja,ambapo dereva anapaswa kuwa na lesini ya uendeshaji wa chombo pamoja na Ile ya latra ya ufanyaji wa biashara ya usafirishaji mtandaoni hapa nchini.
"dereva au abiria atapaswa kupakua aplikesheni ya swiftpack na Kisha kujisajili bure kabisa na kuanza kuitumia. Hata hivyo shirika la Posta kupitia swiftpack limewataka madereva kutumia huduma ya swiftpack kwa kujikwamua kiuchumi kwani haina gharama kubwa katika uendeshaji wake ambao ni bure kabisa kwa Kila mtumiaji ambaye hatotumia bando lake kuita bodaboda wala bajaji,bali atalipa tu nauli ya kupata huduma.
Naye Mwenyekiti wa chama hicho,Renfred Madiko amesema shirika la Posta limekwenda kuondoa changamoto ambazo bodaboda wanazipitia hasa za matumizi ya kimtandao,kwa baadhi ya kampuni nyingine za uagizaji usafiri mtandaoni ambazo hukata makato makubwa kwao,jambo ambalo limekuwa likiibua migogoro baina yao,hivyo kupitia mfumo wa swiftpack sasa usafirishaji umerahisishwa.




Comments