DKT. NEEMA MAJULE: MAJI YASIWE KWENYE MAKARATASI TENA, TUFANYE UTAFITI
DKT. NEEMA MAJULE: MAJI YASIWE KWENYE MAKARATASI TENA, TUFANYE UTAFITI
Dodoma - Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma, Dkt. Neema Majule, ameishauri Serikali kuongeza uwekezaji katika tafiti za maji na mazingira ili kuhakikisha miradi ya maji inatoa matokeo ya kudumu kwa wananchi.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni, amesema bado wananchi wengi wanaendelea kuishi kwa matumaini ya upatikanaji wa maji licha ya kuwepo kwa miradi mbalimbali.
“Maji yasiwe kwenye makaratasi tena. Maji ya Ziwa Victoria tunayatarajia sana, lakini tufanye utafiti wa miamba na mabadiliko ya tabianchi ili tuwe makini na matumizi pamoja na mazingira,” amesema.
Dkt. Majule amesisitiza kuwa tafiti za kisayansi ni muhimu katika kuhakikisha miradi mikubwa ya maji inakuwa endelevu na inaendana na hali halisi ya mazingira.
Aidha, ameonya kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaweza kuathiri upatikanaji wa maji endapo hatua za kitaalamu hazitachukuliwa mapema.



Comments