KILIBA AWATAKA VIJANA KUTOTUMIWA NA WANAOTAKA KUIHARIBU TANZANIA.

 KILIBA AWATAKA VIJANA KUTOTUMIWA NA WANAOTAKA KUIHARIBU TANZANIA.


Mwenyekiti wa taasisi ya mama asemewe Taifa,Geofrey Kiliba amewataka Vijana kutokushiriki katika harakati za kisiasa zinazolenga kubomoa na kudhoofisha maslahi ya vijana hapa nchini.

Kiliba ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam ambao amesema kuwa vijana ni hazina kubwa ya Taifa na endapo itarubuniwa na wanasiasa wasioitakia mema Tanzania basi inaweza kuwa na madhara makubwa.

Amesema Umma wa vijana unapaswa kuelimishwa na kutobebeshwa ajenda za kuliharibu Taifa,kwani watakapoliharibu hawatakuwa na sehemu nyingine ya kukimblia.

"Wamekuwa wakiwahadaa vijana eti wasiwaamini viongozi wao waliowachagua kwa taratibu na katiba ambayo imekuwa ikiaminika siku zote hivyo vijana wasikubali kuhadaika" amesema.

Amesema mambo wanayoyafanya wale wanaowarubuni vijana kuingiza Taifa katika machafuko hayakubaliki na yakifumbiwa macho yanaweza kuigharimu Tanzania hivyo vijana wasidanganyike.


Hata hivyo kuhusu Mjadala wa vijana kuwezeshwa katika awamu mbalimbali za uongozi Kiliba  amesema atakuwa balozi kwa fursa za kiuchumi zinazowekwa na Serikali kwa vijana. 

Amesema Ubalozi wake utajikita katika kubaini,kutangaza na kusambaza uelewa kwa vijana sambamba na kugawa maarifa ya fursa hizo kwa kuondoa upotoshaji miongoni mwa vijana.

Amesema Juhudi kubwa  zimefanywa na Serikali tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu baada ya Rais kuunda wizara ya maendeleo ya vijana ambayo iko chini ya ofisi ya Rais ambayo imeanza kutoa mikopo kwa vijana kote nchini  inaonyesha umuhimu na kusisitiza umuhimu wa maslahi ya vijana ni ishara tosha kuwa Serikali inawathamini vijana.

Comments