NJOMBE YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI
NJOMBE YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI
Njombe - Mkoa wa Njombe umetangaza rasmi fursa mpya za uwekezaji katika sekta ya madini baada ya kubainika kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali za madini ambazo bado hazijatumika ipasavyo, huku wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wakialikwa kuwekeza katika utafiti, uchimbaji na uongezaji thamani wa madini hayo.
Wito huo umetolewa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Lucas Mlekwa, wakati akizungumza katika mahojiano maalum na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma cha Tume ya Madini kinachoshiriki Kikao Kazi cha 21 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini kinachoendelea mkoani humo.
Mhandisi Mlekwa amesema tathmini za kitaalam zinaonesha kuwa wilaya za Njombe, Ludewa, Makete na Wanging’ombe zina utajiri mkubwa wa madini yenye thamani ya kiuchumi, licha ya mengi yake kutokuwa yameendelezwa kikamilifu.




Comments