SEHEMU YA KICHA CHA JAMES TEMBA YAPATIKANA,POLISI YAMTIA MBARONI MGANGA
Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limetangaza kupatikana kwa sehemu ya kichwa iliyokosekana kwenye kiwiliwili cha aliyekuwa mwanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM),James Temba ambaye alipatikana akiwa ameuawa na kutupwa kwenye eneo la mto msimbazi April 30 mwaka huu.
Jeshi hilo limetangaza kupatikana kwa sehemu ya kichwa hicho eneo la Kitunda Kibeberu jijini Dar es salaam kikiwa kimefukiwa ardhini huku likimshikilia mganga wa kienyeji Saidi Ally maarufu kama Side na kufanya idadi ya waliokamatwa mpaka sasa kuhusiana na mauaji hayo kufikia Watuhumiwa watano.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam muda mfupi iliyopita,kamanda wa polisi wa Kanda hiyo, SACP Jumanne Muliro amesema jeshi hilo likishirikiana na mamlaka nyingine za kisheria na kisayansi limepelekea kufanikisha kupatikana kwa sehemu hiyo ya kichwa ambapo taratibu zinakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria zikiendelea kuchukuliwa
"baada ya upelelezi wa kina na wa kitaalam tulifanikiwa kupata sehemu ya kichwa iliyokosekana katika kiwiliwili na tumemkamata mtu mwingine mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji na kufanya idadi ya Watuhumiwa kufikia watano" amesema
Mnamo April 30,2026 jeshi hilo lilianza uchunguzi wa kina wa mauaji ya mwanafunzi huyo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine.
Jeshi hilo limewashukuru wananchi na mamlaka nyingine za kisheria na kisayansi kwa kufanikisha kupatikana kwa kichwa hicho huku likitawaka wananchi kuwa watulivu wakati vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi,na pia limelaani vikali mauaji hayo.



Comments