JKT YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA BIDHAA ZA KILIMO NA UVUVI SABASABA,JAVINUNIA

Na PrayGod Thadei,Dar

 JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha bidhaa za kilimo na uvuvi   kwenye Maonyesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (DITF) yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.


Akizungumzia na waandishi wa Habari mara baada ya kutokea tuzo hiyo,Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Sabasaba Kitaifa JKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, amesema tuzo waliyoipata JKT katika maonesho hayo,siyo tu ni ushindi,bali ni chachu kwao kuendelea kufanya vizuri zaidi na zaidi katika Kila maonesho watakayoshiriki.

"sisi kama jeshi la kujenga Taifa tumejivunia sana na inaonyesha kwamba,tunatambulika kwa Tanzania hii sisi tunafanya vizuri na hata miaka iliyopita tumeendelea kuwa washindi kwa bidhaa zetu mbalimbali na hata mwaka jana tulishinda kwenye eneo la furniture na mwaka huu tulkamua kushiriki kwa upande wa kilimo na tutaendelea kuzalisha bidhaa bora" amesema ili Kila mwaka tuwe washindi"

Amesema siri kubwa ya mafanikio ya ushindi huo ni kufuata maelekezo yanayotolewa na Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa  ambaye mara nyingi amekuwa  akivielekeza  vikosi na shirika la uzalishaji mali na jeshi la kujenga Taifa kufanya vizuri kwa kuzalisha bidhaa bora. 

Aliongeza kuwa mafanikio haya yanadhihirisha dhamira ya JKT katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza uchumi kupitia kilimo na uvuvi kwa vijana, huku akiwataka Watanzania kuunga mkono bidhaa za ndani.

Aidha kuhusu kutekeleza dira ya Taifa ya maendeleo ya 2050 amesema kuwa dira hiyo imeelekeza wazi fursa mbalimbali ikiwemo kilimo na ufungaji na jeshi la kujenga Taifa limekuwa moja ya wadau ambao wanatekeleza dira hiyo kwa vitendo kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali za biashara ikiwemo za Chakula,Kilimo na samani za nyumbani na maofisini.

Maonesho ya sabasaba yanaendela katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam kuanzia June 28 Hadi Julai 13,2026.

Comments