TANZANIA BEACH LOFEGUARDS YAADHIMISHA SIKU YA KUZUIA KUZAMA,YATOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM

 


Na Mwandishi wetu Dar es salaam 

Taasisi ya Tanzania beach lifeguard kwa kushirikiana na chama cha mchezo wa kuogelea nchini na wadau wengine wameadhimisha siku ya kuzuia uzamaji duniani huku ikijidhatiti katika utoaji elimu.


Katika kuadhimisha siku hiyo inayoadhimishwa Leo Julai 25 duniani kote,taasisi hiyo imeendesha mafunzo kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi  wenye ulemavu ili kuwajengea uwezo wa kujiokoa inapotokea wamezama majini.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mwandaaji wa maadhimisho hayo ambaye ni Mkurugenzi wa Tanzania beach lifeguard Bi Amina Mfaume amesema maadhimisho hayo yenye kauli mbinu isemayo "mtu yoyote anaweza kuzama lakini mtu asizame" inayoashiria umuhimu wa kujiokoa na kuokoa majini.

"kwa mwaka huu tumeamua kuwapa mafunzo watoto wenye mahitaji maalum kwani tunaamini wao ndio wapo kwenye risk kubwa sana kutokana na majanga ya maji ndo maana Leo tunawapa mafunzo hapa juu ya namna ya kuogelea na kujiokoa" amesema.

Kwa upande wake afisa tarafa wa tarafa ya Kariakoo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, katika maadhimisho hayo Bw Adrian Kishe ameipongeza taaisi hiyo kwa kuandaa mafunzo hayo kwa wanafunzi wa makundi maalum kwani yatawasaidia namna ya kujiokoa katika majanga ya maji.

Ameongeza kuwa,kama Serikali bado inaendele kuunga mkono jitihada za utoaji wa elimu ya kujiokoa na majanga ya maji kwa kuhakikisha jamii inapata elimu stahiki juu ya majanga hayo ambapo taasisi ya Beach lifeguard imeonesha mfano mzuri ambao kama Serikali inaunga mkono.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa kuogelea nchini Tanzania amesema maadhimisho hayo ni dira dhidi ya kupunguza matukio kwa watu kuzama majini kutokana na kukosa elimu stahiki itakayowafanya kujiokoa pindi majanga yanapotokea.

Comments