Kutana na mwanaume mwenye wake 12 na zaidi ya watoto 100 mpaka wengine amewasahau na kujikuta akimtongoza bintiye

KUTANA NA MWANAUME MWENYE WAKE 12 NA ZAIDI YA WATOTO 100 WENGINE AMEWASAHAU NA KUJIKUTA AKIMTONGOZA BINTIYE.


Togbui Asilenu, mkulima hodari wa umri wa miaka 80 kutoka Ghana anazidi kuwaduwaza walimwengu kutokana na idadi kubwa ya watoto na anataka kuongeza idadi yake.
Asilenu ana wake 12, na watoto zaidi ya mia moja kufikia sasa, na bado angetaka kuongeza idadi yao.
Mzee Asilenu akiwa na wanae wanaomfuata nyuma.








Akiongea na mwanahabari wa TV3 cha nchini humo, Asilenu alidai kuwa hata ampate mwanamke wa kuoa, atamuoa na 
apate watoto naye.

"Hata leo nikipata dada wa kupendeza leo hii, nitamuoa na nipate watoto zaidi. Wanaume hata wakiwa wazee wanaweza pata watoto. Na mie nina uwezo wa kuzalisha," Alisema Asilenu 

Ila cha kushangaza ni kuwa mmoja kati ya wanawe na alisema kuwa mzee huyo hawajui watoto wake wote na hata siku moja alipokutana na binti mmoja mrembo na kuamua kumtongoza ndipo binti Huyo alipomkumbusha kuwa ni mwanaye.

Inadaiwa kuwa licha ya kuwa na watoto wengi wanaodhaniwa kufika 100 ila mzee huyo amekuwa baba mzuri kwa familia na mtoto wake wa kwanza ana miaka 40 huku yule wa mwisho akiwa na mwaka 1.



Comments