CHUO KIKUU ZANZIBAR CHAJIPANGA KUDAHILI WANAFUNZI WAPYA 2020/2021

.CHUO KIKUU ZANZIBAR[ZU] , CHAJIPANGA KUDAHILI WANAFUNZI WAPYA 2020/2021

Banda la chuo kikuu cha Zanziba katika maonyesho ya vyuo vikuu yanayofanyika jijini Dar es salaam.




Dar es salaam
Na  mwandishi wetu,

Wahitimu wa kidato Cha sita wameshauriwa kujiunga na vyuo vikuu vinavyotoa elimu bora kwa mwaka wa masomo 2020/2021 ili waweze kupata elimu itakayo wasaidia kuweza kujiajiri wenyewe.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya mnazi moja na Kaimu Makamo Mkuu wa chuo Utawala chuo kikuu Cha Zanzibar (ZU) Prof Moh'd Makame  Haji 

Amesema kuwa, Chuo kikuu Cha Zanzibar University (ZU) kimeanzisha program maalum( inchubation) ya kufundisha stadi za maisha na ujasiliamali ili kuwapa uwezo wahitimu wa chuo hicho kujiajili.

Aidha alisema ili kukabiliana na ongezeko la wahitimu wasio na ajira ZU inaendelea na program yake hiyo ambapo amesema imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwapa mwanga vijana wanaohitimu kuondoa mawazo ya kuajiliwa.

Aidha Prof Makame aliendelea kusema   kwamba chuo hicho kikuu Cha Zanzibar pia kinatoa program maalum kuwasaidia wahitimu wa ngazi za astashahada na stashahada kupata sifa za kujiendeleza na elimu ya chuo kikuu.

Profesa huyo aliendelea kusema kuwa Chuo hicho kimefanikiwa kutoa wataalamu wa ujuzi mbalimbali ambao wanahudumu Serikali na sekta binafsi.

Aidha aliendelea kufafanua kuwa kutokana na ubora wa chuo hicho,kimekuwa kikipokea wanafunzi mbalimbali kutoka ndani na nje ya bara la afrika hivyo kimekuwa na mafanikio makubwa.

Mwisho

Comments