WHO yahimiza watanzania kuchanja chanjo ya Covid 19.

 

WHO yahimiza watanzania kuchanja chanjo ya Covid 19.

Watanzania wamehimizwa kuendelea kuchanja chanjo ya Covid 19 kwa ajili ya kujiepusha na ugonjwa huo ambao umeua watu wengi duniani.

Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mtaalam wa Chanjo kutoka Shirika la Afya la Dunia upande wa Tanzania,(WHO) Dkt William Mwengee,wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema watu wengi wakichanja itapunguza usambaaji wa ugonjwa huo.

Aidha Dkt Mwengee amesema ugonjwa huu ni wamlipuka hivyo njia pekee kwa watanzania kujiepusha nao ni kuchanjwa ili kuweza kukabiliana na madhara yake.

Aidha, amewasihi Watanzania wasisubiri mpaka madhara ya ugojwa huo yawe makubwa ndio waanze kuchanjwa kwani kufanya hivyo kutafanya virusi hivyo kusambaa.

“Ni vyema watu wakapata chanjo kipindi hiki kuliko kusubiri kusikia kuwa ugonjwa umesambaa sana halafu watu wakachanje itakuwa haisaidii sana kama wakichanja saivi”Amesema Dkt.Mwengee.

Akitoa takwimu ya idadi ya idadi ya watu waliochanjwa,Dk Mwengee amesema mpaka sasa zaidi ya watu bilioni 6.5 duniani kote wamechanjwa ambapo jumla dozi bilioni 6.5 zimeshatolewa.

Hata hivyo,Dkt Mwengee amesema kwa Upande wa Bara la Afrika ni asilimia 3 ya watu ndio wamechanjwa na chanjo ya Uviko 19 na kudai idadi hiyo ni ndogo.

Comments