SHIRIKA LA NYUMBU KIBAHA KUANZA KUZALISHA NGUZO ZA UMEME ZIZIZOPATA KUTU,LAJIVUNIA MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA.
SHIRIKA LA NYUMBU KIBAHA KUANZA KUZALISHA NGUZO ZA UMEME ZIZIZOPATA KUTU,LAJIVUNIA MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA.
Brigedia Jenerali Hashim Yusuf Komba ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Tanzania Automotive Technology Center (TACT),Kamanda wa Kikosi Cha Nyumbu Project kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani |
waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiendelea kupata maelekezo. |
Brigedia Jenerali Hashim Yusuf Komba ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Tanzania Automotive Technology Center (TACT),Kamanda wa Kikosi Cha Nyumbu Project kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani |
Shirika la Tanzania Automotive Technology Center TATC-NYUMBU limesema liko katika hatua za
kusimika mitambo mipya kwa ajili ya kuanza kuzalisha nguzo za umeme za chuma
zizizopata kutu kufuatia serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia
Suluhu Hassan kulipatia shirika hilo kiasi cha shilingi bilioni 9 katika mwaka
wa fedha 2021/22.
Akizungumza na waandishi wa Habari kutoka vyombo
mbalimbali vya habari waliotembelea
shirika hilo ili kujionea utekelezaji wa majukumu yake,Mkurugenzi mkuu wa
shirika hilo la TATC-Nyumbu,Brigedia Jenerali Hashim Komba amesema kuwa hayo
yamejiri baada ya shirika kuandaa mpango mkakati wake wa kipindi cha miaka 10
ambao Rais Samia aliupitisha hivyo fedha hizo bilioni 9 ambapo bajeti yake ni bilioni 25 zimeasaidia shirika hilo katika
Nyanja mbalimbali.
Ameongeza kuwa shirika la TATC-Nyumbu limeingia makubaliano
na shirika la umeme Tanzania,Tanesco kuwajengea nguzo za umeme na vifaa vingine
mbalimbali hivyo mitambo hiyo itakaposimikwa itaisadia serikali kupitia shirika
hilo kutotumia fedha nyingi katika uagizaji wa nguzo hizo za umeme ambazo
zitakuwa zinazalishwa hapa nchini.
Aidha ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa shirika hilo
ambapo mwaka 1977 ulianza kama mradi wa Nyumbu ambayo yalikuwa maono ya Baba wa
Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Julius Nyerere na baadaye December
14 mwaka 1984 ambapo lilibadilishwa kutoka kuwa mradi na kuwa shirika ambalo
litasaidia katika kuendeleza ukuaji wa kiteknolojia hapa nchini kwa kufanya
utafiti wa kiteknolojia kwa kuhuisha na kusanifu mitambo mbalimbali ambapo
mpaka sasa pia shirika hilo lina mradi wa mtambo wa kusindika nyuzi za
katani,mradi wa kutengeneza mkaa utokanao na taka za majumbani na udongo
mfinyanzi ambao utasaidia katika utunzaji mazingira.
Ndugu waandishi wa habari ambao leo mmetutembelea shirika
letu pia linazalisha vifaa mbalimbali vya shirika la maji la Dawasa na pia
tumetengeneza mashine za kisasa za ubanguaji na uokaji wa korosho,sambamba na
kutengeneza mashine ya kukamua juice ya ndizi na pia tumebuni gari la nyumbu ikiwemo
la kubeba wanajeshi,maji na mchanga na pia tumetengeneza gari la kijeshi la
kubeba deraya la kimapigano ARV na
tunendelea na usanifu ili kuwa na magari ya kibiashara na magari haya
yataipunguzia serikali gharama za kuyaagiza nje ya nchi alisema Brigedia
Jenerali Komba.
Hata hivyo shirika la TATC nyumbu pia lina mradi wa
kutengeneza magari ya zimamoto ambapo tayari limeshayakarabati magari 11
kutokana na mkataba wao na jeshi la zimamoto na uokoaji na sasa wanaendelea kuyaunda magari mapya
matatu ambayo uundaji wake umefikia katika hatua nzuri.
Aidha majukumu ya shirika hilo pia kwa mujibu wa mkurugenzi
wake Mkuu ni pamoja na kutoa ushauri wa kiuhandisi ambapo walitoa ushauri kwa
benki kuu ya Tanzania BOT katika ununuzi
wa mashine ya kuhesabu pesa na tayari wameingia ushirikiano na shirika la
maendeleo ya utafiti wa kilimo TARI ili kutengeneza mitambo ya kuchakata miwa
ya wakulima ili kusaidia miwa yao isiharibike na upatikanaji wa uhakika wa
sukari ambapo utafiti ili kuanza mradi huo unaendelea.
Hata hivyo Brigedia Jenerali Komba ameongeza kuwa shirika
hilo limefanya usanifu wa vifaa mbalimbali ikiwemo kutengeneza breakblocks za
shirika la reli Tanzania TRC,Uzalishaji wa vipuri katika sekta ya madini,vipuri
vya magari na chemba za majitaka na pia hufanya ukaguzi wa mitambo
inayonunuliwa na serikali kupitia wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa
ambayo ni mitambo ya kijeshi na pia hutoa huduma za kiufundi JWTZ na Dawasa na
pia ndilo shirika lililobuni na kutengeneza mageti ya Ikulu ya Chamwino iliyopo
jijini Dodoma na pia limefanikiwa kufanya utafiti wa teknolojia mbalimbali hapa
nchini na linaunga mkono sera ya viwanda ya serikali ya awamu ya sita kwa
kuanzisha viwanda mbalimbali ikiwemo cha misumari na tofali,huku likiitaja
changamoto ya ukosefu wa fedha za niradi yake kulingana na uhitaji sambamba na
utumiaji wa baadhi ya mitambo ambayo ni chakavu.
Aidha limeiomba serikali kupitia wizara ya ulinzi na jeshi
la kujenga Taifa waendelee kutoa fedha za maendeleo ya shirika hilo huku
likiwataka watanzania kuiendeleza amani waliyo nayo kwani ni tunu kubwa ya
Taifa letu.
Nao baadhi ya waandishi waliotembelea shirika hilo akiwemo
Judith Chao wa televisheni ya mtandaoni ya Spark TV ameishukuru wizara ya
ulinzi kwa kufanikisha ziara hiyo ya wanahabari kutembelea shirika la Nyumbu na
kuzitaka wizara nyingine kuwa na ziara kama hizo ili kuwajengea wanahabari
uwezo wa kuziandika vyema habari katika Nyanja mbalimbali.
‘’kiukweli nilikuwa sifahamu zaidi kuhusu shirika hili zaidi
ya kulisikia tu lakini leo nimetembelea na kuona mengi sana hasa uundaji wa
magari na nimefarijika kuona gari aina ya Mac12 liliotengenezwa hapa nchini na
tumeambiwa walianza kutengeza kuanzia toleo ya Mac 1 baada ya kuanzishwa kwa
shirika hili hivyo sisi kama wanahabari tumejifunza mengi hapa na tutayaeleza
kwa watanzania kupitia kazi yetu kama waandishi’’alisema Judith Chao wakati
akizungumza na mtandao huu baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ya wanahabari
Comments