MRADI WA HEET WAZINDULIWA,KUNUFAISHA VYUO 14 NCHINI.

 

MRADI WA HEET WAZINDULIWA,KUNUFAISHA VYUO 14 NCHINI.


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa mradi wa maboresho ya elimu juu jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk.Francis Michael akizungumza kuhusiana na mradi wa maboresho ya elimu ya Juu (HEET) jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizindua mradi wa HEET jijini Dar es Salaam.




Dar es salaam.

Katika kuendelea kuboresha sekta ya elimu hasa kwa vyuo vikuu hapa nchini katika kuhakikisha wahadhiri wake wanapata ujuzi wa hali ya juu,serikali kupitia wizara ya elimu imezindua miradi wa HEET ambao utavinufaisha vyuo 14 kote nchini.

Swali akizungumza wakati wa uzinduzi wa miradi huo wa miaka mitano uliofanyika leo jumanne septemba 13,2022,Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa mradi huo utakuwa mwarobaini kwa  kuhahakikisha unawawezesha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya hapa nchini nje ya nchi Ili kusaidia kutoa elimu ujuzi yenye kiwango bora kuendana na soko la ajira kimataifa.

Waziri Prof Mkenda amesema kupitia mradi huu mahususi pia unakwenda kusaidia Wahadhiri kwenda kusoma katika nchi mbalimbali ikiwemo Denmark,Ufaransa,Ubelgiji, Ili kusaidia kuongeza ubora wa Elimu na lazima ianzie juu ndipo ishuke sekondari hadi shule za msingi kwani dunia Sasa hivi imebadikika kinachohitajika ni ujuzi zaidi.

Aidha ameongeza kuwa kupitia mradi huo utasaidia vyuo vya Tanzania kuzalisha wahitimu wenye ubora unaokubalika ulimwenguni kote kwani wahadhiri watapewa mafunzo nje ya nchi ambayo yatawapa mbinu za kuzalisha wahitimu hao wa vyuo vya elimu ya juu

“Duniani kote wanazungumzia suala la elimu hii inatokana na changamoto ya kuwa na wahitimu wengi lakini wanaoshindwa kujiajiri kutokana na kutokuwa na ujuzi ukitazama vyeti wanavyo lakini digree za kutosha lakini mwanafunzi inashindikana kuajiajiri hivyo Wahadhiri waliopata fursa kwenda kusoma njee wakihitimu wanaokuja kubadilisha mtazamo”amesema Waziri

Hata hivyo, Waziri amesema Mradi huo ni mkubwa na ni wa kipekee ambao umekuja kutoa hamasa na kusukuma Tanzania katika suala zima la elimu ikiwa ni pamoja na uboreshajiwa miundombinu ya vyuo ikiwemo mitaala.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael amewataka wasimamizi wa mradi kuhakikisha fedha zikizotolewa za mradi zinatumika katika mlengo uliokusudiwa kwani ikibainika kuna ujanja ujanja watakaohusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amebainisha kuwa fedha zikizotolewa jumla ya dola Milion 425 sawa na Bilioni 972 Ambazo zimetolewa na Benki ya dunia ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu Kwa lengo la kuboresha elimu ya juu hapa nchini.

Naye Mwakilishi kutoka benki ya Dunia Preeti Arora ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na mtazamo chanya wa kuboresha elimu Ili kuendana na mahitaji ya Soko la ajira la kimataifa hivyo watahakikisha wanashirikiana nao began kwa bega pale watakapohitajika.


Comments