DIWANI KATA YA MZIMUNI APONGEZA HATUA YA RAIS SAMIA KUHUDHURIA MKUTANO CHADEMA, ASEMA MWANAMKE NI MTU MWENYE HADHI YA DARAJA LA 1.
DIWANI KATA YA MZIMUNI APONGEZA HATUA YA RAIS SAMIA KUHUDHURIA MKUTANO CHADEMA, ASEMA MWANAMKE NI MTU MWENYE HADHI YA DARAJA LA 1
NA PRAYGOD THADEI
Diwani Lyoto ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea na kutaka kufahamu masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika kata ya Mzimuni.
"Mimi kama mimi katika maisha yangu mwanamke ni mtu wa hadhi ya daraja la 1 kwani Rais Samia amedhihirisha kuwa mwanamke ni mtu mwenye huruma na ambaye anapenda maridhiano"alisema diwani Lyoto.
Amesema kuwa haijawahi kutokea tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini Kiongozi wa juu wa nchi na chama cha mapinduzi CCM kwenda kwenye mkutano wa chama cha upinzani hivyo hatua hiyo imeandika historia ya ajabu ambayo imeonyesha kukua kwa demokrasia nchini.
Aidha diwani huyo ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka miwili tangu kuingia madarakani kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan yamefanyika mambo mengi makubwa ikiwemo kuendeleza miradi mikubwa ya kimkakati iliyoachwa na mtangulizi wake hayati Dkt John Pombe Magufuli.
Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa kuzalisha umeme wa Bwawa la mwalumu Nyerere,mradi wa mabasi ya mwendokasi,reli ya kisasa ya SGR pamoja na kuboresha elimu ili watoto wa kitanzania wapate elimu katika mazingira bora.
"nchi yoyote isiyompa thamani mwanamke kamwe haiwezi kuendelea kwani wanawake ni hazina kubwa na ni watu muhimu na wa kutegemewa katika jamii hivyo Rais Dkt Samia amedhihirisha hilo kwa yale yote aliyofanya mpaka sasa ikiwemo kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ya kisiasa"alisisitiza diwani Lyoto.
Kuhusu maendeleo ya kata ya Mzimuni diwani huyo alisema wameboresha sekta ya elimu ambapo Kwa sasa wanafunzi wa shule za kata hiyo wanapata chakula Cha mchana jambo ambalo limeenda sambamba na Ujenzi wa majiko, sehemu ya kuhifadhia chakula na vyombo vya kupikia pamoja na kuweka kontena maalum la kuhifadhia vyombo hivyo Kwa gharama zake kama diwani huku mzazi akichangia shilingi 1000 tu ya chakula.
Aidha amesema kuwa kama diwani mwenye kupenda maendeleo amejenga kuta kwenye shule zote 3 za serikali za kata ya Mzimuni ili wanafunzi wasome Katika mazingira yenye utulivu pamoja na kununua mashine ya photocopy ili kurahisisha kazi za walimu ambao pia hivi karibuni anatarajia kuanzisha mradi utakaowapa motisha walimu hao kando ya mishahara yao.
Hata hivyo diwani Lyoto ameiomba serikali pia kuangalia namna bora ya kuajiri walimu wenye ueledi ili kuboresha kiwango Cha elimu kwani siyo kila mtu anaweza kuwa Mwalimu.
Kuhusu suala la Afya katika kata hiyo diwani huyo alisema kuwa Zahanati ya kata hiyo imeboresha mazingira ya utoaji huduma ambapo Kwa sasa wanapata dawa za kutosha ambapo na yeye kama diwani pia ameajiri daktari Mmoja, muuguzi pamoja na mtaalamu wa maabara ambao anawalipa mshahara yeye ili wasaidiane na madaktari wengine wa serikali katika zahanati hiyo.
"kiongozi wa ukweli siyo yule anayegombe au kutaka uongozi ili apate kitu Bali yule ambaye anataka kutatua kero za wananchi wake na kufanya vitu vya maendeleo" aliongeza diwani Lyoto.
Comments