SHIRIKISHO LA MACHINGA TANZANIA KUBADILI KATIBA YAO,LAWATAKA MACHINGA KUSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024.

 SHIRIKISHO LA MACHINGA TANZANIA KUBADILI KATIBA YAO,LAWATAKA MACHINGA KUSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024.




Na Thadei PrayGod
Umoja wa Shirikisho la Machinga Tanzanania umesema utabadili katiba yake kufuatia kuwepo kwa mapungufu kadhaa.


Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa umoja wa Shirikisho la Machinga Tanzania (SHIUMA) Steven Lusinde Jijini Dar Es Salaam leo September 11,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kufuatia kikao cha siku Saba kilichofanywa na umoja huo.

Amesema kuwa umoja huo baada ya kujulishwa na ofisi ya msajili wa mashirika juu ya mapungufu hayo wameamua Kuja na kamati ambayo itazunguka nchi nzima katika kufanya marekebisho hayo.

Aidha ameongeza kuwa katibu wa kamati hiyo Ni mwenyekiti wa umoja wa Shirikisho la Machinga,Mkoa wa Dar Es Salaam.

Amesema Kama wamachinga wanaamini serikali ya DKT Samia Suluhu Hassan inawajali na wanaamini serikali itakuja na vitambulisho vya wamachinga ambavyo vitakuwa vimeboreshwa kwa kuwekwa taarifa zote muhimu za Machinga atakayechukua kitambulisho hicho.

"Sisi tunamuunga mkono Rais Dkt Samia na Kamishna Mkuu wa TRA Tanzania kuwa tutakuwa walipa Kodi Wazuri ili kuchangia Pato la Taifa na kuwaelimisha wengine kuhusu kulipa Kodi"amesema Silinde.
 
Hata hivyo katika hatua nyingine,amewataka viongozi wa Mikoa mingine kujenga ofisi kwa ajili ya Machinga Kama ambavyo Machinga wa Dar Es Salaam tayari wamejenga ofisi yao ambayo itakuwa msaada mkubwa kwao ikiwemo kuanzisha Saccos kwa ajili ya wamachinga.

Aidha amewataka pia Machinga wote nchini kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu sambamba na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka mwaka huu,kote nchini ili kuchagua viongozi bora na kuongeza kuwa umoja huo una imani kubwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Katibu wa shirikisho hilo amegawa rasimu za katiba ya Shirikisho hilo kwa viongozi mbalimbali wa Mikoa na makatibu wa Shirikisho hilo na kuwataka wakaisome kwa kuwashirikisha wanachama wao ili watengeneze katiba Bora.

Comments