Skip to main content

BoT YAWATAKA WANANCHI KUKOPA KWENYE TAASISI ZENYE LESENI, yatoa mafunzo kwa Wahariri na waandishi wa habari kuhusu Mikopo mtandaoni

 

BoT YAWATAKA WANANCHI KUKOPA KWENYE TAASISI ZENYE LESENI, yatoa mafunzo kwa Wahariri na waandishi wa habari kuhusu Mikopo mtandaoni





Na Mwandishi Wetu

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka Watanzania kuchukua mikopo kwenye Taasisi zilizo na leseni ya kutoa huduma hiyo.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha (BoT)  Mary Ngasa Wakati wa mafunzo kwa Wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu huduma ya Mikopo mtandaoni.

Amesema kuwa BoT inaendelea kutoa mafunzo ya sheria ya huduma ndogo za fedha pamoja na kanuni zake ili kuwapatia uwezo watoa huduma waweze kuendesha biashara yao kwa ufanisi na kuzingatia haki ya mlaji.

Ngasa amesema kuwa hadi kufika Novemba 2024 wamefanya ukaguzi kwa watoa huduma ndogo za fedha daraja la pili ili kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

Amesema kuwa Taasisi 300 zimefanikiwa kukaguliwa, huku taasisi zilizokutwa na mapungufu ya sheria, kanuni na maelekezo ya BoT zimechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kupewa onyo pamoja na kupunguza riba.

Awali wakati akifungua mafunzo hayo, Kaimu Meneja Huduma Ndogo za Fedha BoT, Dickson Gam imesema BoT itaendelea kutumia rasilimali ili kuhakikisha sekta ndogo ya fedha inakuwa kwa kasi na kuleta tija kwa wananchi kwa kupata huduma bora na kuondokana na umaskini.

Amesema kuwa BoT itaendelea kuhakikisha sekta ya fedha inakuwa thabiti, imara na stahimilivu ili kuwawezesha  shughuli za uchumi.

Gama amesema kuwa watahakikisha wanawatambua watoa huduma wote katika sekta ya fedha kwa njia ya mtandao  ili kuongeza utulivu.

Amesema kuwa ni jukumu la BoT kusimamia huduma ndogo za fedha nchini,  hivyo kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari wataendelea kuwajengea uwezo ili wawe kiunganishi kati  ya benki kuu na jamii kwa ujumla.

“Ukuajiwa wa haraka sekta ndogo ya umesababisha changamoto  kadhaa ikiwemo  masuala  ya kimaadili, riba kubwa, gharama kubwa za mikopo na kukosekana kwa taarifa muhimu” amesema  Bw. Gama.

Amesema kuwa licha ya kuwa na changamoto kadhaa  wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ili watoa huduma  wafanye kazi kwa na manufaa ya wananchi.

Mikopo ya mitandaoni ni mikopo inayotolewa kwa njia ya kidigitali kama vile Applikesheni za simu, tovuti ambayo inapatikana kwa haraka jambo ambalo limeonekana kupendwa na watu wengi, kuongezeka kwa kasi ya mikopo ya mitandaoni imetokana na ukuaji wa teknolojia pamoja na upatikanaji wa haraka wa mikopo ukiwa mahali popote

Comments