ELIMU BILA MALIPO MSAADA KWA WATANZANIA WENGI
ELIMU BILA MALIPO MSAADA KWA WATANZANIA WENGI
#KAZIINAONGEA
Serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya kiongozi mwenye dhamira ya kumwondolea umasikini Mtanzania, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanikisha kuendeleza utoaji wa huduma ya elimu ya msingi bila malipo, hali iliyowawezesha Watanzania wengi kupeleka watoto wao shule.
Ikumbukwe kuwa dhana ya Elimumsingi Bila Malipo inawezesha utoaji wa Elimu kwa Mwanafunzi yeyote bila Mzazi au Mlezi kulipa ada wala michango ya fedha katika shule.
Utozaji wa ada au michango mbalimbali shuleni kwa mwanafunzi ilikuwa ni kikwazo kikubwa hasa kwa Wazazi au Walezi wasio na uwezo.
Kikwazo hicho kilisababisha baadhi ya wanafunzi wasiolipa michango au ada kutohudhuria au kuacha Shule.
Katika kipindi cha kuanzia April, 2021 hadi Februari, 2024 jumla ya Shilingi Trilion 1.1 zimetolewa na Serikali ya Awamu ya Sita na kutumwa Shuleni kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Elimumsingi Bila Malipo.
Fedha hizo ni kwa ajili ya ruzuku ya uendeshaji shule, fedha za chakula cha wanafunzi, fidia ya ada (Bweni na Kutwa) na posho za madaraka kwa wakuu wa Shule na Maafisa Elimu Kata.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye aliyefanya mapinduzi katika Elimu bila ada kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita wananufaika na mpango huu.
Kwa sasa kila mwezi Serikali inatoa bilioni 33 ambapo awali ilikua ikitolewa bilioni 29, ongezeko hili la shilingi bilioni 4 kila mwezi limewawezesha Watoto ambao walikua wanashindwa kuendelea na masomo yao ya kidato cha Tano na Sita kwa kukosa fedha sasa wote wako darasani.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa muhtasari wa mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia tangu aingie madarakani uliotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
#KAZIINAONGEA
- Get link
- X
- Other Apps
Comments