itel yazindua simu mpya ya kisasa A80,yashirikiana na Airtel Tanzania Tanzania,wateja wake Sasa 'kuikopa'

 itel yazindua simu mpya ya kisasa A80,yashirikiana na Airtel Tanzania Tanzania,wateja wake Sasa 'kuikopa'




Na Praygod Thadei.

KAMPUNI ya Itel  Mobile kupitia chapa yake maarufu duniani ya itel kwa kushirikiana kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo wamezindua simu mpya ya kisasa ya Itel A80 .

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa simu hiyo iliyofanyika Leo Novemba 12,2024 jijini Dar Es Salaam Meneja masoko na Mawasiliano wa kampuni ya Itel Mobile Tanzania Bi Sophia Msafiri amesema kuwa simu hiyo mpya ya kisasa ni miongoni mwa simu bora kwa Sasa hapa nchini ambapo inakaa na chaji kwa muda mrefu zaidi pamoja na kuwa na kioo kikubwa cheye inch 6.7 ili kumpa mtumiaji utulivu wakati anaitumia.

"Simu hii pia imekuja na mtandao wa 4G ambapo mteja ataendana na Kasi ya mtandao na baadaye pia zitakuja nyingine za 5G pale ambapo mazingira ya mtandao wa 5G yatakapokidhi hapa nchini na ina ukubwa ambao mteja ataweka vituo vyake vingi huku ikija na kera Kali yenye Mega pixel hadi 13 kwa kamera ya nyuma na Mega pixel 8 kwa kamera ya mbele" amesema Bi Sophia.


Amesema simu hiyo imekuja na nafasi kubwa ya kuhifadhi data ya GB 138+GB 8 ili kuhakikisha watumiaji wake wana uhuru wa kuhifadhi maudhui yao kwa urahisi na itapatikana maduka yote ya itel na Airtel hapa nchini kwa mkopo au pesa taslimu (cash).

"kupitia ushirikiano huu,wateja wa mtandao wa Airtel watapata ofa maalum itakayowawezesha kufurahia huduma za internet kwa gharama nafuu wanapokuwa na itel A80" Amesema.

Kwa upande wake,Meneja mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania,Jennifer Mbuya amesema kuwa ushirikiano thabiti baina ya kampuni hizo mbili ndiyo uliopelekea uzinduzi wa simu hiyo ambayo inaonyesha ari ya Airtel Tanzania katika kupunguza mgawanyiko wa kidijitali nchini kupitia teknolojia suluhishi kwa bei nafuu.

Amesema kuwa simu hiyo itapatikana kwenye maduka yake yote ya Airtel hapa nchini ambapo mteja ataipata kwa kulipa hela taslimu (cash)au kwa mkopo huku akilipa kwa awamu ambapo mteja ataanza na kianzio Cha Shilingi 55,000 na Kisha kulipa 12,00 Kila siku mwaka nzima.

"Ushirikiano Wetu na itel utaongeza matumizi ya Simu kwa watumiaji wa Airtel kote nchini kwa kuchanganya vipengele vya kisasa vya Itel na mtandao bora wa Airtel wenye Kasi zaidi"amesema.

Nao baadhi ya mabalozi (social influencers )wa kampuni ya itel Mobile akiwemo Nancy Moshi amesema kuwa simu hiyo ina ubora wa hali ya juu hivyo Watanzania wanapaswa kuzinunua bila kuwa na shaka yoyote.

Comments