TAMISEMI YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI WA MITANDAO YA KIJAMII,ni kuhusu kanuni uchaguzi Serikali za mitaa 2024

 


 SERIKALI imesema inatambua Umuhimu wa vyombo vya Habari  vya kidijitali na itaendelea kushirikiana na Kila mwanahabari.

Hayo yamesemwa na naibu katibu Mkuu ofisi ya Rais,tawala za Mikoa na Serikali za mitaa,TAMISEMI Dkt Grace Maghembe alipokuwa akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa Habari jijini Dar es salaam kuhusu kanuni za uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.


 "Tunafanya hivi kwa kutoa semina hii kwa waaandishi wa Habari wa mitandao ya kijamii ili kuwapa haki wananchi kujua umuhimu wa kushiriki uchaguzi na viongozi ambao watawachagua"amesema na kuongeza

"Ndiyo maana tumewaita ninyi ili elimu mtakayopata hapa mkawape wananchi na waelimike kwani watanzania wengi wanapenda kupata habari kupitia digital media"

Ameongeza kuwa Tamisemi inatambua kuwa kuwajengea uwezo waandishi wa Habari kutapelekea taarifa sahihi juu ya uchaguzi kuwafikia wananchi kwa kutoa taarifa za uhakikia,zenye kuaminika na kwa wakati.

"Tunatambua kuwa nyie mnanguvu na kupitia nguvu yenu naamini mtapeleka taarifa za uhakika na kuondoa taharuki kwenye jamii" amesema.

Hata hivyo amevitaka Vyombo vya habari hasa vya mitandaoni vitoe taarifa sahihi kwa wananchi ambao wanakwenda kufanya maamuzi ya kuwachagua viongozi na ambazo zitachochea Uzalendo,mshikamano,umoja wetu na sera za wagombea kwa kuzingatia usawa kwa vyama vyote.


Comments