Skip to main content

WAANDISHI WA HABARI ZA MITANDAONI 'WAKAA MEZANI' NA TAMISEMI,NI KUHUSU KANUNI ZA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

 

 WAANDISHI WA HABARI ZA MITANDAONI  'WAKAA MEZANI' NA TAMISEMI,NI KUHUSU KANUNI ZA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI Dkt. Grace Magembe akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii kuhusu Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024.


Habari mbalimbali katika picha kwenye mafunzo hayo.

NA MWANDISHI WETU

KUELEKEA Uchaguzi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetoa mafunzo kwa Wanachama wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) kuhusu Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024.

Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika leo Novemba 13, 2024 jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa kutambua nguvu ya mitandao ya kijamii katika kuhabarisha umma.

"Tunatambua umuhimu wa Digital Media katika kuhabarisha wananchi, ndiyo maana tumeamua kukutana nanyi leo ili tuweze kuwapa uelewa kuhusu Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa," amesema Dkt. Magembe.

Kwamba Watanzania walio wengi kwa sasa wanapenda kupata habari kupitia mitandao ya kijamii (Digital Media) na kwamba kundi la waandishi wa habari za mitandao ya kijamii ni kubwa na linatambulika na Serikali.

Hivyo Dkt. Magembe amesema lengo la mafunzo hayo ni ili waandishi wa habari za mitandaoni waweze kutumia kalamu zao katika kutoa taarifa za uhakika na kweli kuhusu uchaguzi huo, sambamba na kuwaelimisha wapiga kura kutambua umuhimu wa kufanya maamuzi sahihi katika kuchagua viongozi sahihi kwa maendeleo yao.

Hata hivyo amewataka waandishi hao wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na kuhakikisha wanaepuka kutoa taarifa zenye taharuki na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia uzalendo kwa kuunganisha jamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUMIKITA Shabani Matwebe amewataka Wanachama wake kuanzia sasa kuhakikisha wanahabarisha wananchi kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Amewataka wafanye kazi kwa uzalendo mkubwa na kwamba wakifanya kazi kwa ukubwa na Wizara nyingine zitaona umuhimu wao na kuwashirikisha katika kazi zao.

Ametumia fursa hiyo kwa kuishukuro Ofisi ya Rais, Tamisemi kwa kutambua nguvu ya mitando ya kijamii na kuamua kuishirikisha JUMIKITA kuelekea Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Comments