Posts

Showing posts from January, 2025

NANI KUMRITHI KINANA CCM?NI JANUARI 18-19 MWAKA HUU,NI KATIKA MKUTANO MKUU WA CHAMA HICHO

DKT. KAZUNGU APONGEZA TANESCO KWA USIMAMIZI BORA WA MITAMBO YA UMEME NCHINI.

WASICHANA WAONGOZA MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA PILI 2024

Huu hapa Utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo nchini Tanzania kuanzia saa 3 usiku wa Leo

SERIKALI KUFUNGUA MAWASILIANO SIMANJIRO-MANYARA

SERIKALI KUFUNGUA MAWASILIANO SIMANJIRO-MANYARA kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inajipanga kufungua mawasiliano kwa kuunganisha Barabara ya Langa-Mkuu na Msitu wa Tembo katika Kata ya Msitu wa Tembo- Ngorika kuelekea Ngange wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara. Kaimu Meneja wa Tarura Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Naftari Chaula amesema hayo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi na matengenezo ya barabara wilayani humo. Mhandisi Chaula amesema Barabara hiyo imekuwa ikikumbwa na mafuriko pamoja na sehemu nyingine kutofunguliwa kutokana na kuwa na makorongo mengi yaliyosababishwa na mvua nyingi. Amesema kwa mwaka huu wa fedha wanatarajia kukamilisha ujenzi wa madaraja kwa zaidi ya asilimia 70 na tayari mkandarasi yupo eneo la ujenzi akiendelea na uchimbaji na upangaji wa mawe na kwamba kukamilika kwa ujenzi huo kutafungua mawasiliano kati ya Kata ya Ngorika na Msitu wa Tembo na kuwezesha usafirishaji wa mazao ya uvuvi kutoka Bwawa la Nyumba ya Mungu. “Wananchi wamekuwa wakipata shida sana katika shughuli za usafirishaji wa mazao ya uvuvi, bidhaa nyingine za kilimo na hata wananchi wa Ngorika kwenda Hospitali ya Kata ya Msitu wa Tembo na Hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro na mahali kwingine kwaajili ya matibabu” alisema Mhandisi Chaula. Kwa upande wao wananchi wa Kata hiyo wameishukuru Serikuli kupitia Wakala hiyo kwa kuwapelekea mradi huo ambao wanasema utasaidia kuondoa changamoto walizokuwa wakikutana nazo. Thomas Sokoine Mkazi wa Kijiji cha Londoto Kata ya Msitu wa Tembo amesema kujengwa kwa daraja katika korongo hilo kutasaidia wananchi wakiwemo watoto kutokukwama tena kuvuka upande wa pili. Kwa upande wake Robert Juma dereva wa lori la mizigo amesema barabara hiyo imekuwa ni changamoto sana hususani wakati wa mvua na kumshukuru Rais Samia kwa kuwapelekea mradi huo wa ujenzi wa makalavati akisema anaamini utawaondolea changamoto wanayokumbana nayo ikiwemo kusitisha shughuli za usafirishaji hasa katika kipindi cha mvua. Naye Jorum Yohana Mkazi wa Msitu wa Tembo amesema maeneo yao yalikuwa ni hatarishi sana kutokana na maji kuleta adha kubwa kwa wananchi na kuishukuru Serikali kwa kuwawekea lami kipande cha Kilometa 1 na kuongeza kuwa serikali imeongeza fedha kwa kuwajengea makalavati, hivyo wanaamini barabara hiyo ikikamilika itawasaidia katika shughuli za kilimo, ufugaji na biashara zitaendelea kuinuka na hivyo

WATAKAOHUSIKA KUDHOOFISHA JITIHADA ZA SERIKALI PORI LA AKIBA KILOMBERO KUSHUGHULIKIWA : MHE. DUNSTAN KYOBYA

Huu hapa Utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo nchini Tanzania ikiwa Leo tumeanza mwaka mpya wa 2025